
Kwa mujibu wa Alikiba, ajali hiyo ilitokea juzi Jumapili alfajiri (saa 11) ambapo gari dogo walilokuwa wakisafiria lilipinduka na kuacha njia eneo la Mikumi, hali iliyosabisha abiria nane waliokuwa ndani yake kujeruhiwa vibaya.

“Nahisi chanzo cha ajali ni dereva kusinzia kwani sote tulikuwa tumelala, tukashtukia gari likiacha njia na kupinduka. Namshukuru Mungu wote tumesalimika. Mimi sikuumia sana ila wenzangu walijeruhiwa na kukimbizwa kwenye Hospitali ta Mkoa wa Morogoro, mpaka sasa wote wamesharuhusiwa baada ya kupata matibabu na hali zao kuwa nzuri,” alisema Ali Kiba.
No comments:
Post a Comment