PIGA KURA BSS 2ND CHANCE; ANDIKA BSS 05 KISHA TUMA KWENDA NO. 15747.

Tafuta hapa

Monday 4 July 2011

Na Shakoor Jongo
Wimbi la baadhi ya masupastaa wa Bongo kuzaa watoto bila kuwa kwenye ndoa au kuishi na mwanamume, sasa limeonekana kuwa fasheni huku wengi wao wakiwa wanawaficha waliowapa ujauzito, Risasi Jumamosi limebeba mkoba wa uchunguzi.

Utafiti wa kina umeonesha kwamba, baadhi ya mastaa hao wamekuwa wakibeba ujauzito bila kujali wanamume wanaowapa, ili mradi awe na mshiko.

Katika tafsiri ya kiimani kutoka kwenye vitabu vitakatifu, mastaa hao wanazini kwa vile, maandiko yanaelekeza kuwa, mwanamume au mwanamke anatakiwa kufunga ndoa kabla ya kujamiiana.

Kwa mujibu wa msanii mmoja anayeshika kasi kwenye gemu la maigizo kwa sasa Bongo (jina tunalo), mastaa wengi wa kike wameamua kuzaa bila ndoa kwa sababu wanaume wa kuwaoa hawapo na wao umri unakwenda.

Akiendelea kuweka wazi siri hiyo ya mastaa kuzaa kwa fasheni, msanii huyo alisema kuwa, pia wapo mastaa ambao wanaamua kunasa mimba ili kujihakikishia kwamba wao si wagumba.

“Wapo (mastaa) waliamua kubeba mimba ili kujipima kama wazima au tasa, lakini wengine ni wale ambao umri umekwenda lakini hawaolewi, nao wameamua kuzaa ili wawe na watoto japo wa dawa,” alisema msanii huyo.
Risasi Jumamosi lina orodha ya mastaa wa Bongo ambao wamezaa bila kuolewa na wengine wakiwaficha ‘mababa’ wa watoto wao.
Maureen Gislary; Mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2005, mwaka huu alijifungua mtoto wa kike aitwaye Milania Fiona huku akikataa katakata kumwanika mzazi mwenzake.

Suzana Chubwa ‘Queen Suzy’; Ni mnenguaji wa Bendi ya FM Academia. Ana mtoto mmoja aitwaye Jackson Junior ambaye inasemekana alizaa na muimbaji wa Bendi ya Mapacha Watatu, Kalala Hamza ‘Junior’. Baba huyo aliwahi kumkataa mtoto. Hawapo katika ndoa.
Nancy Sumari; Miss Tanzania mwaka 2005 (pichani), amejifungua mwaka huu mtoto wa kiume. Naye amekataa kabisa kumtaja baba wa mwanaye akisema ni siri yake, lakini hajaolewa.

Snura Mushi; Ni msanii wa filamu za Kibongo, ana mtoto wa kike aitwaye Talha aliyejifungua mwanzoni mwa mwaka huu. Yeye pia hajawa wazi kumwanika baba wa mtoto wake huyo akisema ni siri yake. Hayuko kwenye ndoa.

Husna Iddi ‘Sajenti’; Ni Kimwana Manywele 2008. Yeye ana mtoto wa kike aliyezaa na mwimbaji wa Bendi ya The African Stars, Charles Gabriel ‘Chalz Baba’. Mtoto anaitwa Carinal Charles Gabriel.

Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’; Yeye ni staa waTamthiliya ya Jumba la Dhahabu. Amezaa mtoto mmoja na msanii mwenzake, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’. Hawako kwenye ndoa na wala hawakuwa na mpango wa kuoana.

Isabella Mpanda ‘Bellah’; Ni Miss Ruvuma 2008. Alijifungua mtoto wa kiume mwaka 2010 na kumwita Obama. Amewahi kutamka kuwa, baba wa mtoto wake ni kigogo wa Wizara ya Ujenzi jijini Dar es Salaam, lakini amekuwa akikataa kumtaja jina.

Joyce Kiria; Presenta wa Vipindi vya Bongo Movies na Wanawake Live. Mwezi Juni, 2011 alijifungua mtoto wa kiume kwa njia ya upasuaji akiwa ameachika kwa mumewe, Nelson Nkongo ‘Dj Nelly’. Kwa sasa ana mchumba lakini haijajulikana lini atafunga ndoa.

Lucy Komba ‘Lona’; Ni staa wa filamu Bongo, ana mtoto aitwaye Strom. Tofauti yake na baadhi ya mastaa wenzake wenye watoto, yeye anamtaja Francis Mbasha kuwa ndiye baba wa mtoto huyo. Lakini hawaishi pamoja na wala hawana mpango wa kufunga ndoa.

Aisha Mohamed Mbegu ‘Madinda’; Ni mnenguaji wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’. Licha ya kuwa na watoto wawili, kila mmoja na baba‘ake, hivi karibuni alitamka kuwa, anataka kuzaa mtoto mwingine, lakini hajaolewa.

No comments:

Post a Comment