PIGA KURA BSS 2ND CHANCE; ANDIKA BSS 05 KISHA TUMA KWENDA NO. 15747.

Tafuta hapa

Monday 4 July 2011

BONGO STAR SEARCH 2011 HII HAPA

Bongo star search 2011,inakuja kwa kishindo kikubwa kwa kuwapa nafasi nyingine washiriki waliopita ambayo itakuwa na jina la BSS 2ND CHANCE. Mchuano utahusisha washiriki wa Bongo star search Kutoka mwaka 2006 hadi 2010.

image
Bongo star search 2011,inakuja kwa kishindo kikubwa kwa kuwapa nafasi nyingine washiriki waliopita ambayo itakuwa na jina la BSS 2ND CHANCE. Mchuano utahusisha washiriki wa Bongo star search Kutoka mwaka 2006 hadi 2010.

Historia ya Bongo star search
Bongo star search ilianza mwaka 2006,ambapo iliweza kuwapa nafasi vijana wa kitanzania wenye vipaji vya kuimba mziki,Azimio Hili la BSS limeweza kuleta mafanikio makubwa ya vijana wa kitanzania kwa muda wa miaka mine sasa.Kutoka mwaka 2006 mpaka 2010 BSS ilichukua ziara mikoa mbalimbali ya Tanzania kwaajili ya kutafuta Vipaji vya mziki.Washindi wa Bss miaka mine(4)iliyopita walipata zawadi nono ambazo ziliwasaidia kunyanyua mfumo wa maisha yao.

Mafanikio ya BSS kutoka mwaka 2006-2010
Bss imeweza kufanikisha hazma yake ya kutimiza ahadi zake kwa kutoa zawadi zote kwa washindi wa BSS miaka yote,na mafanikio hayo yamepelekea washindi kubadili mfumo wa maisha yao ,kwa ujumla.Pia zawadi zimekuwa zikiongezeka kila mwaka kuanzia BSS ilipoanza hadi sasa.

Maandalizi ya Bongo star search
Kila mwaka Bongo star search imekuwa ikifanya mchujo kwa kuchukua washiriki mbalimbali kila mkoa Tanzania na kutafuta vipaji vilivyo bora kabisa.
Mwaka 2011,majaji wa Bongo star search walikaa chini na kupitia mikanda yote ya BSS ZiliZopita toka mwaka 2006 hadi 2010,na hatimaye kuwapata washiriki 30 ambao walikuwa na vipaji vizuri zaidi.
Muundo wa Bongo star search 2011

Washiriki watakuwa thelathini(30)na watachukuliwa kutoka mwaka 2006 hadi 2010.
Kutokana na mfumo huu,Bss imeamua kuchukua washiriki waliofanya vizuri zaidi katika kila mwaka.

Malengo.
Malengo ya Bongo star search 2011 ni kuwapa nafasi nyingine washiriki wa miaka ya nyuma yaani 2ND CHANCE na kuwafanya wajulikane kwa mara nyingine,Pia watambulike kuwa wana vipaji ambavyo vinaweza kuwa hazina ya nchi yetu ya Tanzania.

Mipango ya BSS 2011
Benchmarkproductions mmiliki wa Bongo star search,imeamua kuleta mabadiliko katika Bss mwaka huu 2011.kwa kuwapa washiriki wa miaka iliyopita nafasi nyingine ya kuonyesha vipaji vyao na pia kuwaonyesha Tanzania kuwa bado tunavipaji ambavyo vilizalishwa na BSS miaka ya nyuma na bado havijapata nafasi ya kuonekana.

Kwa mara nyingine,washiriki wa Bongo star search 2011 watakuwa 30(thelathini)na watachujwa mpaka kufikia 14 kwaajili ya mipambano ya michujo ya kila wiki.
1. Kutakuwa na ufunguzi wa Bongo star search 2011 ambao utahusisha mafanikio ya BSS kutoka miaka mine (4)ya nyuma hadi sasa,Lengo ni kusheherekea Miaka mitano ( 5 )ya Bongo star search na pia miaka hamsini (50)ya Uhuru wa Tanzania
2.Hatutakuwa na usahili mwaka huu kwasababu tutawachagua washiriki wa BSS miaka ya nyuma kutoka 2006 hadi 2010.Hivyo badala yake tutafanya usajili wa washiriki 30 ambao watarushwa kwenye televisheni ya ITV kwa muda wa wiki mbili(2)baada ya hapo wananchi watawapigia kura washiriki 20 tu ili kuingia kwenye michuano
3.Baada ya kupata kura za washiriki 20,watapelekwa kwa majaji watatu(3)wa Bongo star search ambao watachujwa na kupatikana washiriki 14 ambao wataingia kwenye nyumba tayari kwa mashindano ya kuchujwa kila mwisho wa wiki
4.Kutakuwa na matukio mbalimbaili katika maandalizi ya Bongo star search kama,Press release na washiriki thelathini(30) watarushwa kwenye vyombo vya habari na magazeti kwaajili ya kutoa hamasa za kura kwa washiriki hao
5.Mapema Baada ya mchujo wa pili wa washiriki,ambao watakuwa 14,na watakuwa na mafunzo mbalimbali ambayo yatakuwepo kwa muda wote huo wa mashindano.mafunzo hayo ni kama, usafi,na Mziki.
7.Kutakuwa na vipindi 14 vya Bongo star search ambavyo vitakuwa vinaoneshwa kila wiki,ambapo kutafanyika mchujo kwa kila wiki.
8.Mashindano ya mwisho yatahusisha washiriki wanne (4)tu ambao watachuana vikali LIVE stajini ambapo watakuwa wakichujwa mpaka kupatikana mshindi wa kwanza(1)
9.Washindi watatu watapewa zawadi ,na mwaka huu zawadi ya mshindi wa kwanza itakuwa nono zaidi ya miaka mine (4)iliyopita
10.Mfumo wa kura wa Bongo star search Kila mwaka ni, Kura za majaji ni asilimia 60,na wananchi(wapigakura)ni asilimia 40.
11.Faina

No comments:

Post a Comment