PIGA KURA BSS 2ND CHANCE; ANDIKA BSS 05 KISHA TUMA KWENDA NO. 15747.

Tafuta hapa

Monday 4 July 2011

MAAJABU JAMANIIIIIIII.....!

JE, umewahi kuona bilula “inayotema” maji bila kuliona bomba lake linakotokea?
Kwa ufahamisho tu ni kwamba, “bilula” ni kile kidude kilicho mwisho wa bomba linalobeba maji ambacho hutumiwa kulifunga au kulifungua ili liweze kutoa maji.

Neno hilo ni  Kiswahili murua japokuwa cha zamani.
Turejee kwenye swali letu: Umewahi kuliona bomba (bilula) linalotoa maji bila kujua au kuyaona maji hayo yanatokea wapi?

Kama hujawahi kuliona, basi ni hilo linaloonekana katika picha hii.  Bilula hiyo iko sehemu inayoitwa Aqualand, Hispania,  ni moja ya vivutio vikubwa duniani ambapo watu hufurika kwenda kushangaa.  Ni kivutio cha utalii.

Dude hilo ni kubwa na refu kwenda juu ambalo “hutema” maji kwa wingi kama vile yafanyavyo mabomba lukuki, kwa mfano, jijini Dar es Salaam, ambayo hunyonya maji kutoka Mto Ruvu ulioko mkoani Pwani.

Kweli, ni uchawi wa mchana kweupe!
Hata hivyo, ukweli ni kwamba: Hapa hapana uchawi wowote.   Katika sehemu inayotoa maji kuna bomba lililofichwa na maji hayo ambalo hunyonya maji hayo kutoka chini, likayarushwa juu halafu yakateremka tena kama vile “yanatemwa” na bilula hiyo!

Inafurahisha, au siyo?  Si uchawi, hata wewe unaweza kufanya hivyo!  Ni uchawi wa kisomi.

No comments:

Post a Comment