PIGA KURA BSS 2ND CHANCE; ANDIKA BSS 05 KISHA TUMA KWENDA NO. 15747.

Tafuta hapa

Sunday, 3 July 2011

NYUMBANI LOUNGE

ALHMIS YA MWISHO WA MWEZI JUNE, 30 NA MENGINEYO


Dully Sykes alipita na Wooyoooo wiyoo wayoo woyooyo wio wayooo BongoFlava!!!!



TID hali kadhalika






Wadau flani hivi ambao wao hawana neno kutokea kwenye Blog

Na hadithi ikaishia hapo

NYUMBANI LOUNGE

USIPATE TABU KUFIKIRIA LUNCH UTAKULA WAPI JUMATATU.....

Ni kweli kabisa kuwa hata vya hivi huwa tuna serve, Jaribu, hutajutia.



Jumatatu NYUMBANI lOUNGE kwenye Buffet la Mchana kutakuwa na: Supu ya Beef Cubes
Ugali wa Muhogo

Wali wa Nyanya

Nyama ya Ng'ombe "Kidali"

Chicken Peri-peri "Kuna Option ya kutokuwa na Pilipili pia"

Samaki wa Mchuzi wa nazi

Kisamvu

Maharage

Fruit Salady

na Pilipili ya Kupikwa

Friday, 1 July 2011

KUTOKA MAGAZETINI

AGNES: Napenda nikiwa faragha na mpenzi wangu wote tuwe bwiii


Wiki hii kupitia safu hii tunaye sistaduu ambaye ni msanii wa filamu. Licha ya usanii, pia mwanadada huyu amejipatia umaarufu kutokana na kuuza sura kwenye video za mastaa mbalimbali wa muziki hapa Bongo. Anaitwa Agnes Gerald (pichani).

Alizaliwa Aprili 23, 1988 kwenye hospitali ya Mkoa wa Mbeya na akasoma Shule ya Msingi na Sekondari ya Sangu. Hayo ni kwa uchache tu, zaidi kuhusu Agnes, ungana nami katika maswali 10 niliyomuuliza.

TQ: Hili zali la kuuza sura kwenye video mbalimbali umelipataje? Kuna mtu yeyote ambaye anakuunganisha na wasanii hawa?
Agnes: Kwanza ni muonekano wangu lakini pia rafiki yangu mmoja alinikutanisha na baadhi ya wasanii hao na wao wakaona nafaa kuwemo kwenye kazi zao.

TQ: Inasemekana umetokea kwenye familia ambayo imeiva kidini, wao wanachukuliaje hili suala la wewe kuingia kwenye mambo haya ya kuuza sura tena wakati mwingine kwenye mavazi ya kimitego?
Agnes: Mh! Baba yangu hataki kabisa kusikia mambo ya muziki na niliwahi kukosana naye lakini nalazimisha kwa kuwa ni moja ya ajira.

TQ: Mbali na kazi ya kuuza sura, una dili nyingine zinazokuongezea kipato na kuweza kuishi mjini bila wasiwasi?
Agnes: Mimi ni mjasiriamali, nina teksi zangu mbili lakini pia katika siku zijazo nina mpango wa kufungua Super Market.

TQ: Vipi ‘outings’ zako, unapendelea kwenda sehemu gani?
Agnes: Napenda sana kwenda Club kujirusha hasa siku za wikiendi.

TQ: Kuna za chini chini kuwa umewahi kumlegezea Belle 9, hebu funguka katika hili.
Agnes: Siyo kweli bwana, huu ni mtambo mkubwa, mimi na yule wapi na wapi?

TQ: Kabla ya kuanza mechi ya kiutu uzima, unapenda wewe na mpenzi wako muwe katika hali gani?
Agnes: Huwa ‘nainjoi’ sana wote tukiwa tumelewa (Anaangua kicheko).

TQ: Ni kipi unachokumbuka katika mapenzi yako ya utotoni?
Agnes: Ni pale nilipokutana kwa mara ya kwanza na mwanamume. Pia nilipobeba ujauzito nikiwa mdogo hali iliyonifanya nifukuzwe nyumbani na baba.

TQ: He! Sasa ulijifungua au uliichoropoa mimba?
Agnes: Ilibidi nizae, tena mtoto wa kike, anaishi na baba yake huko Kinondoni ngoja nikuoneshe picha (Anafungua simu na kumuonesha mwandishi).

TQ: Dah! Mzuri sana, kwa nini huishi naye?
Agnes: Baba yake amemng’ang’ania kitu ambacho kimenifanya nimchukie mzazi mwenzangu huyo.

TQ: Lakini bado unampenda mwanamume huyo?
Agnes: Hapana kwa kuwa baada ya kunipa mimba alinisaliti, wakati nilifukuzwa nyumbani kwa sababu yake, kimsingi sitaki hata kumsikia.

GLOBAL Ujauzito wa Teddy Kalonga!

Na Mwandishi Wetu
Mwanadada aliyewahi kuwa Mtangazaji wa Televisheni ya Channel 5 kisha akapata zali la kuolewa na Mzungu nchini Marekani, Teddy Kalonga ‘TK’ (pichani)  amewashangaza mashabiki wake kufuatia kuanika picha yake ikionesha kuwa ni mjamzito.

Picha hiyo ambayo pia inapatikana kwenye blog yake inamuonesha TK ambaye pia anajishughulisha na ‘umodo’ akiwa na ‘kitumbo’ ambacho kwa haraka kinaonekana kuwa na zaidi ya miezi minne.

Wakiuzungumzia ujauzito huo, mashabiki mbalimbali wa mwanadada huyo walimpongeza kwa hatua hiyo lakini wakamlaumu kwa kuwaficha hadi mimba yake kuwa kubwa.

“Mimba imempendeza sana lakini mbona katuficha sisi wadau wake? Mungu amjalie ajifungue salama na ikiwezekana apate mapacha,” alisema Karen wa Moshi.

Naye Miriam Simbeyu wa Kinondoni jijini Dar alisema: “Nami sijui nitakuwa lini kama alivyo TK, mimba ni kitu kizuri sana hasa kwa walio katika ndoa…furaha ilioje kwake.”

Staa wa Kiwanda cha Filamu Bongo, Irene Uwoya ambaye hivi karibuni alijifungua mtoto wa kiume, ametoa somo kwa wasanii wenye majina makubwa nchini, kuacha tabia ya kutoa mimba kwa sababu kitendo hicho siyo kizuri, Ijumaa linashuka na mkoba wenye ishu nzima.

Akizungumza na gazeti hili katikati ya wiki hii nyumbani kwao Mbezi, jijini Dar es Salaam alipotembelewa na mwandishi wetu, Irene alisema anamshukuru Mwenyezi Mungu aliyewajalia kupata mtoto huyo ambaye amewatengezea heshima kubwa.
“Kusema ukweli mimi na mume wangu tunamshukuru sana Mungu, ametupa mtoto huyu, naamini amesababisha kuongezeka kwa heshima katika jamii,” alisema Uwoya.

Akaongeza: “Kwa wale wenzangu watoa mimba, nataka wajue ni hatari sana kwani wanaweza kupata matatizo, likiwemo la kutozaa kabisa maishani mwao.”

Aidha, aliongeza kuwa mwanamke anapozaa hupata heshima katika jamii inayomzunguka kwani anaitwa mama, jambo ambalo ni jema.
Irene aliongeza kuwa, kitendo cha kuzaa kinamfanya kuongeza ubize na shughuli za utafutaji wa ‘pesa’ ili kuongeza kipato kwa ajili ya kumlea mwanaye tofauti na mwanamke ambaye hana mtoto.

Akiendelea kutoa ushauri huo, alisema kwamba ikitokea mwanamke akapata ujauzito ambao hakuutarajia asithubutu kuutoa licha ya misukosuko atakayoipata na kuonekana asiyefaa.

“Unajua inapotokea msichana kapata mimba kabla ya kuolewa au akiwa shuleni, ndugu, jamaa na hata jamii itamuona mkosaji lakini hiyo isiwe sababu ya kuitoa kwani mtoto anapozaliwa hupendwa na kila mtu,” alisema Irene.
Kufuatia ushauri huo, Ijumaa liliwaendea hewani baadhi ya mastaa na kuwaambia ushauri huo wa Uwoya na kusikia kutoka kwao ambapo wa kwanza kutoa maoni alikuwa mtangazaji wa runinga Bongo, Maimartha wa Jesse ‘Mai’.

Yeye alisema: “Nikiwa mwanaharakati wa mambo ya wanawake nakubaliana na Uwoya, siwezi kutoa mimba hata siku moja kwani najua madhara yake.”

Mai aliyataja baadhi ya madhara hayo kuwa ni kulegea kizazi au kuharibika kabisa, kuvuja damu kila wakati (internal bleeding), kujiharibia maisha hasa pale unapoingia kwenye ndoa, mwanaume anataka mtoto wewe tayari umeshaharibu kizazi.

Mwanaidi Suka ‘Mainda’;
“Binafsi sijawahi kutoa mimba na sitathubutu kufanya hivyo kwani madhara yake ni kifo, kupoteza fahamu au kutokwa damu nyingi na pia ni kosa la jinai, nawashauri wenye tabia hiyo waache.”

Rehema Fabian, Balozi wa Kiswahili;
“Ukweli nakiri mimi niliwahi kutoa  mimba, lakini roho iliniuma sana nikizingatia kwamba, kitendo hicho kinaweza kusababisha kansa ya kizazi au ugumba. Sababu kubwa iliyonisukuma kufanya dhambi hiyo ni kugundua mwanaume mwenyewe hakuwa na msimamo, nikahisi nitailea peke yangu.”

Rose Ndauka;
“Kwa kweli mimi siyo daktari, siwezi kujua madhara ya kutoa mimba, ila kama mtu kanasa bila kutarajia siyo vibaya kuitoa ili asije akazaa mtoto ambaye atakuja kuteseka duniani.”
Naye supastaa mmoja wa filamu Bongo (aliomba jina lake lisitiriwe ili asijenge bifu na Uwoya) alisema kuwa, anamshangaa sana Uwoya kutoa somo hilo wakati na yeye ni staa.

“Heee! Makubwa! Uwoya ndiyo anasema hivyo? Naye si staa? Ina maana anatoa darasa hilo kwa sababu amepata mtoto, nina hakika hata yeye alishawahi kuchoropoa mimba kabla hajaolewa.
“Tusidanganyane, hapa Bongo hakuna staa wa kike ambaye hajawahi kutoa mimba kabla hajaolewa,” alisema staa huyo.

KUTOKA MAGAZETINI

Msanii kutoka Nyumba ya Kukuza Vipaji Tanzania (THT), Estherlinah Sanga ‘Linah’ (pichani) ameibuka na kusema kuwa, hana mpango wa kutoa penzi kwa mtu yeyote kwa sasa.

Linah alitoa kauli hiyo juzi kati baada ya kuulizwa na paparazi wetu juu ya tetesi kwamba sasa hivi anatoka na kijana anayefahamika kwa jina la Nick wa Pili ambapo kuweka mambo sawa alisema:

“Sijui nisemeje maana hizo habari siyo za kweli, mimi kwa sasa sina mtu yeyote niko singo na wala sina mpango wa kuwa na mpenzi, nimeamua kufanya kwanza kazi zangu za muziki zaidi.”

Linah alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake, Amini Mwinyimkuu kabla ya hivi karibuni kutosana.


Na Mwandishi Wetu
Kwa jicho la juu, warembo mastaa muonekano wao ni bei mbaya a.k.a expensive, wapo wanaovunja benki ili kuwanasa bila kujua siri nzito iliyopo, kumbe asilimia 90 ni bei chee.

Ingawa wapo wenye misimamo yao na wasiozuzuka na ‘usistaduu wa kideoni’, idadi kubwa ya mastaa wanaotibua ‘kitaani’ na kwenye vyombo vya habari ni sababu ya tasnia nzima kuingia doa.

Ijumaa ‘The Udaku Master’, kupitia uchunguzi wake limebaini makundi matatu ambayo warembo hao wameyatengeneza, mosi likiwa la wale wanaojiheshimu (watulivu, wenye msimamo), pili ni la wale bei mbaya ‘expensive’ (kuwapata inabidi ujipinde), tatu lenye memba wengi ni la bei chee.
Ripoti ya Ijumaa pia ina kundi la warembo ambao pamoja na kwamba hawakuwekwa kwenye kundi lolote kati ya hayo matatu lakini tabia na vitendo vyao vimekuwa vikitia ‘kinyaa’ na kusababisha jamii iwashushe hadhi.

WANAOJIHESHIMU
Mastaa ambao mpaka sasa wameonesha msimamo na wanajiheshimu ni Malkia wa Afro Pop Bongo, Judith Wabura ‘Lady Jaydee’,  (aliyepakatwa na mumewe pichani)  mtangazaji nyota aliye pia mwanamuziki, Fina Mango ‘Ndege Mnana’ na staa wa filamu, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’.

Wengine wenye msimamo ambao hawajanaswa na skendo ya aina yoyote mpaka sasa ni mtangazaji Zamaradi Mketema, mrembo aliyetisha kwenye Hip Hop, Zainab Lipangile ‘Zay B’, Miss Tanzania 2007/08, Richa Adhia na Miss Tanzania namba mbili 2006/07, Jokate Mwegelo.
Wapo wengine wanaoonekana wanajiheshimu lakini Ijumaa limewaondoa baada ya kubaini kasoro zao za chini chini, huku baadhi likitaka kujiridhisha zaidi.

BEI MBAYA
Kundi hili, linaundwa na mastaa wenye msimamo kwa wanaume ‘makapuku’ lakini ni wepesi mbele ya wafanyabiashara na wanasiasa wanaojua ‘kukata mpunga’.

Ingawa majina yao yanahifadhiwa kwa sasa, Ijumaa lina orodha ya mastaa 13 ambao wamekuwa wakigawa mapenzi kwa wanaume matajiri kwa matarajio ya kupata malipo makubwa.

Hata hivyo, baadhi yao wamejikuta wakiaibika baada ya kunyang’anywa magari ambayo walihongwa na wanaume kama malipo ya kuwapa mapenzi ya ‘nipe nikupe’.

BEI CHEE
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba, mastaa wengi wanaounda kundi kubwa ni bei chee kwa sababu hutoa penzi ama kwa gharama nafuu au bure ili kutimiza matakwa yao ya kuwa maarufu.
Ijumaa limebaini kwamba, warembo wengi hasa waigizaji, hujirahisi kwa maprodyuza mastaa ili wapate kuonekana kwenye filamu zinazotengenezwa.
Prodyuza mmoja aliliambia gazeti hili hivi karibuni kuwa warembo wengi kabla ya ‘kuuza’ sura kwenye filamu mbalimbali, huwapa ofa ya unyumba baadhi ya maprodyuza.

“Hii ipo wazi kabisa, tasnia inaundwa na watu wengine hatari kabisa. Baadhi yao walikuwa hawajatulia huko mtaani na wengine wameshindwa maisha, kwa hiyo kutoa unyumba kwa prodyuza ili watoke hawaoni kazi.

“Ni wengi sana wanajirahisi. Unaweza kuwaona ni mastaa kwenye filamu lakini nje wanatongoza wanaume ovyo,” alisema prodyuza huyo (jina tunalo).

Ukiachana na prodyuza huyo, hivi karibuni gazeti ndugu na hili, Ijumaa Wikienda liliandika habari ya staa mmoja wa filamu kumpigia simu mbunge wa jimbo moja la Morogoro na kumuomba wawe pamoja.

Mbunge huyo aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, mrembo huyo alikuwa anamheshimu lakini alimshusha thamani baada ya kumtongoza bila aibu.
Aidha, Ijumaa inaifanyia kazi orodha ya mastaa 22 ambao wanatajwa kuwa kimeo kuliko wengine kwa kuwa na tabia ya kutongoza au kujitongozesha kwa wanaume.

KUNDI LINALOCHAFUA TASNIA
Uchunguzi umebaini kuwa, mastaa wanaoongoza kwa skendo, wamekuwa wakichafua hali ya hewa na kusababisha hata wengine wanaojiheshimu waonekane hawana maana.
Staa wa filamu, Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’ anatibua hali ya hewa kutokana na skendo zake za waume za watu pamoja na ile ya kufumwa chumbani akiwa na mchumba wa mtu mwaka juzi.

Aunt alifumwa akiwa na brazameni, Mwilu Mwilola ‘Silvanus’ ambaye alikuwa mchumba wa msanii, Sara Mwakapala. Hivi sasa Aunt na Silva ni wapenzi wa kudumu.
Skendo za Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu kubadili wanaume mara kwa mara na ‘kashkash’ za kukamatwa na polisi, ni baadhi ya vitu vinavyochafua ‘statas’ ya ustaa ndani ya ‘Bongoland’.

Mastaa Jacqueline Pentzel, Jacqueline Patrick, Blandina Chagula ‘Johari’, Sylvia Shally, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na wengineo wengi pia wanatajwa kuwa sehemu ya ‘uchafuzi’ wa hali hewa katika tasnia kutokana na skendo zao za hapa na pale.



Wiki hii tunaye msanii wa muziki wa Bongo Fleva, anaitwa Raheem Rummy Nanji a.k.a Bob Junior (pichani). Jamaa licha ya kuwa Rais wa Masharobaro, anamiliki studio yake ya Sharobaro Records.

Alizaliwa Machi 19, 1989 katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam na kusoma Shule ya Msingi na Sekondari St. Marry’s hapa jijini Dar hadi kidato cha nne.
Zaidi kuhusu mshikaji huyu ungana nami katika maswali 10 ambayo nilimuuliza.

TQ: Ni nani hasa aliyekushawishi kuingia katika fani ya muziki?
Bob Junior: Ni baba yangu kwani hata yeye alikuwa mwanamuziki na katika familia yetu wengi ni wasanii.

TQ: Kuna tetesi kuwa wimbo wa Oyoyo ulitungiwa na Bob Kisouji, hili limekaaje?
Bob Junior: Haa! Bob Kisouji siyo msanii bali ni bosi wangu, hawezi kunitungia wimbo.

TQ: Ni siku gani ambayo hutaisahau maishani mwako?
Bob Junior: Dah! Yaani huwezi kuamini siku ambayo Wema Sepetu alinitukana nililia sana, siwezi kuisahau siku ile.

TQ: Mbali na muziki kuna kazi nyingine ambayo inakuingizia kipato?
Bob Junior: Muziki ndiyo kila kitu kwangu hivyo siwezi kuchanganya na kitu kingine.

TQ: Tugeukie kwenye maisha yako ya kimapenzi, umeoa?
Bob Junior: Sijaoa ila nina mpenzi wangu ambaye siku zijazo huenda tutafunga ndoa.

TQ: Ni maeneo yapi unapenda kushikwa ukiwa faragha na mpenzi wako?
Bob Junior: Akinipumulia masikioni tu basi, natoa kilio cha beberu.

TQ: Nini kilikuvutia kwa mpenzi wako huyo?
Bob Junior: Unajua mimi ndiye wa kwanza kwake, hivyo nilimuonesha mapenzi ni nini, yaani nilivutiwa na upya wake kwenye mapenzi.

TQ: (Swali la kizushi) mademu wanasema wewe ni mtaalamu wa kuzama baharini kutafuta chumvi ni kweli?
Bob Junior: (kicheko) siwezi kuzungumzia hilo maana ni la ndani sana.

TQ: Hebu kuwa muwazi, inadaiwa ulimtaka Wema kimapenzi na ulipomchomekea ndipo akakutukana, funguka sasa.
Bob Junior: Siyo kweli bwana, mimi hanivutii kiivyo.

TQ: Poa Bob Junior, panapo majaaliwa tutaonana siku nyingine.
Bob Junior: Dah! Umenitoa jasho la haja mtu wangu, karibu tena.Wiki hii tunaye msanii wa muziki wa Bongo Fleva, anaitwa Raheem Rummy Nanji a.k.a Bob Junior. Jamaa licha ya kuwa Rais wa Masharobaro, anamiliki studio yake ya Sharobaro Records.

Alizaliwa Machi 19, 1989 katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam na kusoma Shule ya Msingi na Sekondari St. Marry’s hapa jijini Dar hadi kidato cha nne.
Zaidi kuhusu mshikaji huyu ungana nami katika maswali 10 ambayo nilimuuliza.

TQ: Ni nani hasa aliyekushawishi kuingia katika fani ya muziki?
Bob Junior: Ni baba yangu kwani hata yeye alikuwa mwanamuziki na katika familia yetu wengi ni wasanii.

TQ: Kuna tetesi kuwa wimbo wa Oyoyo ulitungiwa na Bob Kisouji, hili limekaaje?
Bob Junior: Haa! Bob Kisouji siyo msanii bali ni bosi wangu, hawezi kunitungia wimbo.

TQ: Ni siku gani ambayo hutaisahau maishani mwako?
Bob Junior: Dah! Yaani huwezi kuamini siku ambayo Wema Sepetu alinitukana nililia sana, siwezi kuisahau siku ile.

TQ: Mbali na muziki kuna kazi nyingine ambayo inakuingizia kipato?
Bob Junior: Muziki ndiyo kila kitu kwangu hivyo siwezi kuchanganya na kitu kingine.

TQ: Tugeukie kwenye maisha yako ya kimapenzi, umeoa?
Bob Junior: Sijaoa ila nina mpenzi wangu ambaye siku zijazo huenda tutafunga ndoa.

TQ: Ni maeneo yapi unapenda kushikwa ukiwa faragha na mpenzi wako?
Bob Junior: Akinipumulia masikioni tu basi, natoa kilio cha beberu.

TQ: Nini kilikuvutia kwa mpenzi wako huyo?
Bob Junior: Unajua mimi ndiye wa kwanza kwake, hivyo nilimuonesha mapenzi ni nini, yaani nilivutiwa na upya wake kwenye mapenzi.

TQ: (Swali la kizushi) mademu wanasema wewe ni mtaalamu wa kuzama baharini kutafuta chumvi ni kweli?
Bob Junior: (kicheko) siwezi kuzungumzia hilo maana ni la ndani sana.

TQ: Hebu kuwa muwazi, inadaiwa ulimtaka Wema kimapenzi na ulipomchomekea ndipo akakutukana, funguka sasa.
Bob Junior: Siyo kweli bwana, mimi hanivutii kiivyo.

TQ: Poa Bob Junior, panapo majaaliwa tutaonana siku nyingine.
Bob Junior: Dah! Umenitoa jasho la haja mtu wangu, karibu tena.            

  

Thursday, 9 June 2011

MIZUNGUKO YA HAPA NA PALE NIKIWA KAMPALA

Pozi muhimu.....!

But hili ni kiboko.....!

muda mwingine huwa napenda kusoma vitabu.....! nani anabisha....?

Ukisoooma ukachoka inabidi kupumzika kama hivi....!

Mh.....hapo chacha!

Buzuku la mchana mchana ha ha ha ha..!

I dnt nid a soldier coz i gat 1!

guess what................? yes ur ryt..!

Kubebwa raha jamani...!

No comment...!

kama KAWA kama DAWA....!

Kukumbatia muhimu, coz wezi wengi siku hizi.....!

Baada ya mizunguko ya kutosha ikabidi tuweke pozi kidogo...!

hili ni sanamu la KWAME NKRUMAH

Monday, 6 June 2011

Show yangu ya mwisho na Machozi Band kabla ya kusafiri...!

Hapa nikiwa stejini...!

Dada jay dee, mwinyi & mimi mwenyewe

Umati wa watu uliokuja kushuhudia Machozi Band jumapili hii..!

Dada lady jay dee akiwa kwa steji

Mashabiki wa Machozi Band wakila bata ndani ya nyumbani lounge huku show ikiendelea..!

Hapa nikiwa na Jonico na Mwinyi