PIGA KURA BSS 2ND CHANCE; ANDIKA BSS 05 KISHA TUMA KWENDA NO. 15747.

Tafuta hapa

Monday, 4 July 2011

Na Shakoor Jongo
CD na VCD zinazomuonesha mshiriki wa Big Brother Amplified 2011, Bhoke Egina akifanya malavidavi na aliyekuwa mwakilishi  wa Uganda, Ernest Wasake imeanza kusambazwa na wafanyabiashara wa mitaani ‘Wamachinga’ jijini Dar es Salaam,” Risasi Jumamosi lina data kamili.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umegundua kuwa Wamachinga wanauza CD hizo kati ya shilingi 2500 na 3,000 na kuzifanya zigombewe kama peremende.

Gazeti hili liliongea na baadhi ya watu walioziona CD na VCD hizo zikiuzwa katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ambao pia walishangazwa na vitendo alivyofanya binti huyo katika Jumba la Big Brother, Afika Kusini.

“Tulikuwa tukisoma kwenye vyombo vya habari lakini hatukuamini kama ni kweli Bhoke amefanya uchafu ule na raia wa Uganda,” alisema Mama Jumaa, mkazi wa Magomeni jijini Dar.
 “Mimi sina ‘king’amuzi’, nimeona katika CD hii, sasa najiuliza hivi alivyokuwa akifanya uchafu ule wazazi wake na ‘boyfriend’ wake walikuwa wakiangalia?” alisema mtu mwingine ambaye jina lake halikupatikana  mara moja.
Baada ya kusikia kauli hizo, Risasi Jumamosi liliwavutia waya baadhi ya mastaa wa Bongo ili kusikia maoni yao kutokana na kitendo hicho alichokifanya Bhoke.
Mcheza filamu maarufu, Vincent Kigosi ‘Ray’: “Nahisi katudhalilisha sana Watanzania, lakini kwa upande mwingine siwezi kumhukumu kwa sababu sina uzoefu wa nyumba ya Big Brother, inawezekana mazingila yanamruhusu kufanya uchafu ule lakini ni bora aliyoyafanya Lotus kuliko uchafu wa Bhoke,”alisema.

Aidha, Ray aliwashauri wawakilishi wa Big Brother nchini kuachana na kuwapeleka akina dada katika mashindano hayo, kwa kuwa hawana historia nzuri tofauti na wanaume.
“Habu angalia alichokifanya Richard Bezuidenhout na Mwisho Mwampamba ambao waliweza kulitangaza vyema taifa,”alisema.

Staa mwingine wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ yeye alisema kitendo alichokifanya Bhoke kimemsikitisha sana kiasi na kuona aibu kama vile amekifanya yeye.
“Kwa kweli Bhoke ametuvua nguo, ule si utamaduni wa mwanamke wa Kitanzania, nilitegemea alivyorudi angeomba radhi, matokeo yake anasema alienda Big Brother kama Bhoke na siyo kuipeperusha bendera ya Tanzania, inasikitisha,”alisema.

Staa mwingine wa filamu, Aunt Ezekiel yeye alikuwa tofauti kidogo pale aliposema kuwa kimaadili ya Kitanzania Bhoke amekosea lakini anayachukulia matendo aliyoyafanya kama ni njia ya kusaka ushindi.
“Sitaweza kumchukia, kwani nahisi alivyokuwa mjengoni alikuwa siyo Bhoke yule tunayemjua siye, kwa hiyo nikibahatika kukiona kipindi chake nitamchukulia kuwa ni mtangazaji na nitakaa na kukiangalia bila ya ‘kumjaji’ vibaya,” alisema.

Staa wa filamu, Mwanaidi Suka ‘Mainda’ alisema: “Kwa kweli siwezi kuongea chochote, kwani sikubahatika vitendo vyake, nitakuwa kama nahukumu kitu nisichokijua, kitendo ambacho ni dhambi mbele ya Mungu.”

Mtangazaji wa Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’: “Kama kuna watu wanamchukia Bhoke, basi mimi ni namba moja, kitendo chake kimetudhalilisha, halafu inaonesha ni mwepesi kwa mwanaume na bingwa wa kutongoza, unajua Bhoke ndiye aliyejitongozesha kwa Ernest? Eti mtangazaji, asituharibie fani yetu,” alisema.

Aidha, Dida alisema kuwa alifahamu kama CD na VCD za uchafu alioufanya zitauzwa na kuongeza kuwa haiwezi kuishia hapo, kwani hata kwenye simu watu wanahamishiana uchafu wake.
Mcheza filamu Jacqueline Pentzel  ‘Jack wa Chuz’:“ Amejidhalilisha, labda kama ni masharti aliyopewa na Big Brother afanye vile mi nitaona ni kawaida.”
Mwingine aliyechangia ni mcheza filamu maarufu, Rose Ndauka: “Kanichefua sana, sijui amelelewa vipi, ningekuwa miye yaani hata nyumbani nisingepokelewa,” alisema.
Msanii huyo alisema kuwa bado hajaiona CD ya uchafu wa Bhoke na kuongeza kama kweli itakuwepo, itakuwa ni aibu yake kwa mara ya pili.
Staa wa filamu, Latifa Idabu ‘Badra’: “Mimi namuona mshamba tu hana lolote, ametudhalilisha sana, umaarufu hautafutwi kama vile.”

Msanii mwingine wa filamu, Zuwena Mohammed ‘Shilole’:” Mi siwezi kusema chochote.”
Akihojiwa na Jarida la iMagazine la Uingereza hivi karibuni, Bhoke alisema: “Siku ile nilikuwa nimelewa sana hivyo siwezi kubisha kilichotokea.” 

No comments:

Post a Comment