Na Shakoor Jongo
Ikiwa ni zaidi ya miaka miwili tangu walipofunga ndoa ya kihistoria, watayarishaji na waigizaji wenye majina makubwa Bongo, Wastara Juma (pichani) na Juma Kilowoko ‘Sajuki’, wamefunguka juu ya changamoto za kimaisha walizopitia katika kipindi hicho huku mwanadada huyo akiahidi kuzaa mapacha.
Akizungumza ‘exclusively’ na The 5Star Paper, Risasi Jumamosi juzikati akiwa njiani kuelekea visiwani Zanzibar ‘kushuti’ filamu yao mpya inayokwenda kwa jina la Kijacho, Wastara aliweka kweupe kwamba, ahadi aliyowekeana na mumewe katika ndoa yao imetimia hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kula wa kupokea mgeni au wageni.
Wastara alisema kuwa, baada ya kufunga ndoa waliingia kwenye misheshe na msoto uliojaa changamoto za kimaisha za kutafuta ‘mahela’ ili kuweka mambo safi kabla ya kupata watoto lakini kwa sasa mambo yametulia na muda si mrefu ndoa yao ‘itatema’.
Alisema: “Jamani katika maisha ya ndoa si kweli kwamba watu wakishaoana wanakimbilia kuzaa, lazima wajiwekee malengo kwanza.
“Watu wanapaswa kujua kuwa, ni muhimu kuandaa mazingira ya huyo mtoto mwenyewe atakayezaliwa.
“Kwa sasa ni ‘full uhakika’, ninaamini haitafika Januari, mwakani na nadhani watakuwa ni watoto mapacha.
“Cha msingi tumuombe Mungu tu kwani muda wowote kuanzia sasa mashabiki wangu watasikia habari mpya za ndoa yangu.”
Baada ya kupata habari hizo njema kutoka kwa wastara huku ikiaminika kwamba kama Januari haitafika, basi malkia huyo wa filamu inawezekana ni mjamzito, Risasi Jumamosi lilimgeukia mumewe Sajuki na kumuuliza kuhusu suala hilo ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Natamani habari hizo za mke wangu kupata mapacha zitimie kwani itapendeza sana wakiwa wa kike na wa kiume.
Sajuki alisema, alipanga kuwa na mahali pake pa kuishi na usafiri wa uhakika hivyo kwa sasa amepata nyumba na gari kwa hiyo kilichobaki ni kusubiria watoto.
Wawili hao walifunga ndoa Mei, 2009 hivyo Mungu akiwajalia watoto mapacha watakuwa wamefunga kazi kwa mastaa ambao wameoa au kuolewa na

No comments:
Post a Comment