PIGA KURA BSS 2ND CHANCE; ANDIKA BSS 05 KISHA TUMA KWENDA NO. 15747.

Tafuta hapa

Monday, 4 July 2011

STAA wa Kibongo aliyejinyakulia umaarufu mkubwa kupitia ngoma ya Hands Across The World, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ amepata ajali ya gari na wacheza shoo wake eneo la Mikumi, Morogoro wakiwa safarini kurejea jijini Dar es Salaam kutokea Mkoani Mbeya walikoenda kupiga shoo, Erick Evarist ana data kamili.

Kwa mujibu wa Alikiba, ajali hiyo ilitokea juzi Jumapili alfajiri (saa 11) ambapo gari dogo walilokuwa wakisafiria lilipinduka na kuacha njia eneo la Mikumi, hali iliyosabisha abiria nane waliokuwa ndani yake kujeruhiwa vibaya.
Hata hivyo, hakuna aliyepoteza maisha kwenye ajali hiyo na Alikiba alipata majeraha madogo huku baadhi ya wacheza shoo wake wakipata majeraha makubwa na kukimbizwa hospitali.

“Nahisi chanzo cha ajali ni dereva kusinzia kwani sote tulikuwa tumelala, tukashtukia gari likiacha njia na kupinduka. Namshukuru Mungu wote tumesalimika. Mimi sikuumia sana ila wenzangu walijeruhiwa na kukimbizwa kwenye Hospitali ta Mkoa wa Morogoro, mpaka sasa wote wamesharuhusiwa baada ya kupata matibabu na hali zao kuwa nzuri,” alisema Ali Kiba.

No comments:

Post a Comment