Na Mwandishi Wetu
Afya ya Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu ina tatizo, mwili wake umetoa majibu na daktari amethibitisha.
Uchunguzi umebaini kuwa Wema anasumbuliwa na ugonjwa unaoitwa Adiposis Edematosa au kwa jina lingine ni Cellulite ambao chanzo chake mara nyingi husababishwa na mpangilio mbovu wa chakula.
Ngozi ya Wema ina mistari mingi hasa mgongoni lakini amekuwa hajui hali hiyo, ndiyo maana anashindwa kujisitiri na kuvaa mavazi yanayomuanika maeneo yaliyoathirika.
Chanzo cha Cellulite ni mabadiliko katika usagaji wa chakula, tatizo ambalo huwakumba wanawake wanaojiachia, hivyo Wema ameingia kwenye kundi hilo.
Kwa ufafanuzi zaidi wa kisayansi, ugonjwa huo pia chanzo chake ni matatizo katika mmeng’enyo na usanisi wa chakula tumboni, ulaji wa kupindukia wa vyakula vigumu vyenye kemikali zinazoshambulia mfumo wa utengenezwaji wa seli za ngozi.
Cellulite pia ni matokeo ya mabadiliko ya ufanyaji kazi wa homoni za kike ambazo husababisha ngozi kukunjamana, sababu za kijenetiki na mzunguko hafifu wa virutubisho vya ngozi kwenye damu.
Kuishi na msongo wa mawazo na hofu za mara kwa mara ni sababu nyingine inayochochea uzalishwaji wa kemikali iitwayo Catecholamines ambayo ikisambaa mwilini husababisha tatizo hilo.
DALILI
Kwa mujibu wa Daktari Abdullah Masoud ambaye amebobea katika tiba ya ngozi, dalili kubwa ya Cellulite ni mwili wa mwanamke kushambuliwa na mistari au mikunjo kwenye maeneo ya mgongoni, mapajani, mikononi na mengineyo.
“Ukishaona mistari juu kwenye mwili wa mwanamke maana yake tishu zake zimeshaharibika na kupoteza mpangilio wake wa kawaida (dimorphic skin architecture), kwa hiyo mara kwa mara huwa tunawashauri wanawake waangalie mpangilio wa maisha yao kwa jumla,” alisema Dokta Masoud.
Aliendelea: “Siyo mistari tu, hilo naomba lieleweke, hata mikunjo ya ajabu ajabu kwenye mwili wa mwanamke hasa kijana ni matokeo ya Cellulite.”
Dk. Masoud alisema: “Unywaji wa pombe kali, uvutaji wa sigara navyo ni tatizo. Naomba wanawake waache, wanaharibu ngozi zao.”
WEMA HAJIJUI
Ijumaa Wikienda limebaini kuwa Wema hajui kuhusu tatizo hilo ndiyo maana amekuwa akivaa mavazi yanayoacha wazi sehemu za mgongo wake ambayo ndiyo uliyoathirika zaidi.
Limebaini pia kuwa Wema ameathirika hata kwenye maungio ya mikono na mabega pamoja na sehemu ya kifuani.
WEMA ZAMANI BWANA!
Gazeti hili baada ya kuona picha za Wema aliyeharibika, lilirudi kujiridhisha kwa kuangalia zile za zamani na kubaini kwamba alikuwa ‘kifaa cha nguvu’ na sasa ni ‘fotokopi’.
Ngozi ya Wema wa zamani ilikuwa laini inayovutia, haikuwa na mistari wala mikunjo, hivyo kumfanya awe mrembo anayestahili kuvuliwa kofia.
WEMA ANAWEZA KUPONA?
Tiba kadhaa zimekuwa zikitajwa kumaliza tatizo hili ingawa wataalamu wameshindwa kuthibitisha ufanisi wake.
Kwa mujibu wa Dokta Masoud, hakuna tiba ya uhakika ya kumaliza tatizo hilo ingawa zipo baadhi ya dawa ambazo zinatajwa kupunguza makali ya Cellulite.
“Mpaka sasa hakuna tiba ya moja kwa moja ya Cellulite ila inashauriwa kwa mtu mwenye tatizo hilo abadili mfumo wa maisha yake na akifuata m
No comments:
Post a Comment