Jamii itambue kuwa mtu anayejifanya mpole kitandani hawezi kufanikiwa. Mwisho atamboa mwandani wake. Mantiki ya kutokuwa na muwajibikaji, hujenga tafsiri upande wa pili kwamba hujisikii inavyotakiwa, au huna hamu ila unatenda kwa kulazimisha.
Mzuka wa kutosha ni kitu muhimu mno unapokuwa faragha. Ndipo mwenzi wako anapoweza kuona mpo pamoja na akaamini kuwa unamtosheleza. Atajuaje kama anakupa raha stahiki ikiwa mwenzako anawajibika wewe umetoa macho kama mjusi kabanwa na mlango?
Hivyo basi, busara ya kwanza ya kitanda iwe ni kuziweka hisia zako kwenye tendo. Akikushika nawe shikika. Usizuie hisia, hebu tekenyeka basi. Unajikausha ili uonekane mgumu, nani alikwambia ugumu una nafasi pale wawili wanapokutana faragha?
Ukweli ni kuwa sanaa ya mapenzi inamuongoza mtu kujua maeneo gani ya kufanyia kazi. Kwa maana mpenzi wako atataka ayabaini maeneo ambayo wewe hukupa mzuka wa kutosha. Sasa atayajuaje kama unajikausha. Unaguswa mahali, wewe unakakamaa mwili mzima ili usioneshe hisia.
Ni mapenzi siyo mateso. Ni mchezo wa kugawana hisia. Mgawie zako naye akugawie zake. Usizibane, ukifanya hivyo utafeli. Mpe urahisi wa kutambua maeneo ambayo yanaweza kukupa raha, naye afanye hivyo kwako ili muweze kwenda sawa.
Winston Churchill, Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, aliyeongoza katikati ya karne ya 20 alisema: “Hakuna binadamu mwenye mafanikio kijamii aliyekosa ‘kashkashi’.” Akasisitiza, mtu ambaye anaishi kwa unyenyekevu na utakatifu akakosa dhambi yoyote, huyo mara nyingi anakuwa hana mchango kwa jamii.
Alimaanisha kiongozi mzuri nyuma ya pazia pengine ni mlevi kupita kiasi. Ana dorasi ya kupenda watu barabarani na kutaka kuingia nao kitandani. Kauli yake naichukua katika eneo kuwa kama hakuna binadamu aliyefanikiwa kijamii lakini akakosa ‘kashkashi’.
Hata kitandani, inabidi uwe na kashkashi. Uoneshe ni kwa namna gani kinachotendeka eneo la tukio kinakuhusu. Tunapaswa kuheshimu wenzi wetu na siyo kuwa wapole.
Unyenyekevu faragha ni kutii kinachofanyika lakini siyo upole, pia papara haihitajiki.
Tunahitaji kutibu papara. Tunapaswa kuitambua miili yetu halafu twende na kasi tunayoimudu. Tuache kujipa mizigo tusiyoiweza. Wengi wanakwenda kwa waganga wa jadi wakidhani wanaumwa kumbe ni wazima.
Laiti kila mtu atakuwa mtulivu na kuheshimu hisia zake, naamini waganga wanaotengeneza fedha kwa kuuza dawa za mapenzi au nguvu za kiume wangefulia. Lakini wanapewa jeuri na watu wanaojiuguza ugonjwa wasiokuwa nao.
Zoezi la faragha linatekelezwa kwa nafasi na kituo, si kurukaruka. Umefika mshindo mara hii, baada ya sekunde kadhaa unajing’ang’aniza kurejea ulingoni. Unadhani kwa kufanya hivyo huyo uliyenaye atakuona upo ngangari. Unajidanganya.
Matokeo yake, badala ya kukuona ngangari ndiyo kwanza unaumbuka. Mwili haukuwa tayari kwa tendo, kwa hiyo papara zako zinakufanya ukutese. Unajitesa mwenyewe. Nyama choma ipo mbele yako, unaitamani lakini jeuri ya kuila huna. Aibu!
EPUKANA NA AIBU HII
Achana na simulizi za kijiweni. Usiendeshwe na tamaa. Himili wasiwasi halafu jiamini kwa kila nukta kisha utaona jinsi unavyoweza kutekeleza shughuli ipasavyo. Zingatia kuwa mapenzi yanahitaji muda wa kutosha. Ukitaka kurudi mara mbili ndani ya dakika 15 ndiyo mwanzo wa kuumbuka.
Mtu bora ni Yule anayechukua muda kufika mshindo mmoja, halafu anapumzika kwa muda wa kutosha kabla ya kurejea ulingoni tena. Umekutana naye, mara dakika tatu umecheua, kabla hujajipanga unataka upande tutani tena. Utachekwa kila siku.
Mapenzi hayakuumbwa ili umkomoe mwenzako.
Itaendelea wiki ijayo.

No comments:
Post a Comment